Thursday, July 26, 2012
MKUU WA POLISI UGANDA ATOA AMRI YA PASPORT YA DR JOSE CHAMELEONE IRUDISHWE HARAKA
Mkuu wa jeshi la polisi nchini Uganda, IGP, Kale Kayihura amewaagiza maofisa wa Tanzania kuirudisha haraka passport ya Jose Chameleone.
Kayihura ametoa amri hiyo alipokutana na Chameleon kwenye kituo cha polisi cha Muyenga mchana wa leo jijini Kampala.
Amesema maafisa wa hapa nchini wamesema passport ya msanii huyo ingewasili baadaye leo na kukabidhiwa kwake mara moja.
Leo Jose Chameleone akiwa na mashabiki wake wameandamana kwenye ubalozi wa Tanzania nchini Uganda kudai arudishiwe passport hiyo iliyokuwa ikishikiliwa na Erick Shigongo kwa madai kuwa meneja wake amemtapeli dola 3500.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment